Tayari rais wa Msumbiji Filipe Nyusi yupo nchini humo kwa ziara ya siku tatu na atafuatiwa na rais wa China Xi Jinping, atakayekuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo kuzuru Rwanda.
Baadaye kati ya tarehe 23-24 mwezi huu Waziri Mkuu wa India Nahedra Modi atakuwa jijini Kigali.
Viongozi hao wanatarajiwa kujadiliana kuhusu ushirikiano wa Rwanda na bara la Afrika kuhusu masuala mbalimbali hasa biashara na usalama.