Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/04 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Salva Kiir na Riek Machar kutia saini mkataba wa amani Alhamisi

media Riek Machar na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir wakati wa kutia saini mkataba wa amani, Mei 9, 2014 Addis Ababa. REUTERS/Goran Tomasevic

Sudan inasema rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar wanatrajiwa kutia saini makubalianio ya awali ya ya kugawana madaraka Alhamisi wiki hii kabla ya mkataba wa mwisho tarehe 26 mwezi huu.

Taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje nchini ya Sudan imesema pande zote husika na mzozo zitatia saini makubaliano ya kugawana madaraka Alhamisi Julai 19, 2018.

Pande hasimu Sudan Kusini zimeafiki kugawana madaraka kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na pande hizo ambapo kwa mujibu wake kiongozi wa waasi nchini humo, Riek Machar atarejeshwa katika wadhifa wa Makamu wa Rais.

Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Al Dierdiry Ahmed,alisema kuwa imeafikiwa kwamba kutakuwepo makamu wanne wa rais; yaani makamu wawili wa rais waliopo hivi sasa pamoja na Riek Machar, na nafasi ya nne ya makamu wa rais atapangiwa mwanamama kutoka kambi ya upinzani.

Itakumbukwa kuwa mrengo wa upinzani nchini Sudan Kusini na serikali ya nchi hiyo walifikia makubaliano katika juhudi za kuhitimisha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Vita hivyo vilianza mwaka 2013 baada ya hitilafu za kisiasa kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake, Machar kusababisha machafuko ya ndani.

Pande mbili hizo hasimu nchini Sudan Kusini zimehusika katika mauaji ya ulipizaji kisasi ambayo yaliibua miganyiko ya kikabila. Makumi ya maelfu ya watu wameuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi kufuatia machafuko hayo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana