Pata taarifa kuu
KENYA-OBAMA-USHIRIKIANO-MAENDELEO

Obama apongeza hatua ya maridhiano kati ya Kenyatta na Odinga

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amepongeza hatua ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuamua kuweka pembeni uhasimu wao na kushirikiana kwa ajili ya umoja wa taifa hilo.

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama huko Kogelo, Kenya, Julai 16, 2018.
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama huko Kogelo, Kenya, Julai 16, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Obama ametoa kauli hii, wakati wa ufunguzi wa kituo cha kukuza michezo na kutoa elimu kwa vijana kinachofahamika kama Sauti Kuu kinachomilikiwa na dada yake Dokta Auma Obama, katika kijiji cha Kogelo, alikozaliwa baba yake, Magharibi mwa nchi hiyo.

Kiongozi huyo wa zamani ambaye amerejea nchini Kenya, kama raia wa kawaida, amesema ushirikiano unaoneshwa na viongozi wa nchi hiyo, ni dalili nzuri ya nchi hiyo kupata maendeleo.

Obama anazuru Afrika Kusini kusherehekea miaka 100 tangu kuzaliwa kwa aliyekuwa rais wa kwanza mweusi nchini humo Nelson Mandela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.