Pata taarifa kuu
KENYA-OBAMA-MAENDELEO-UCHUMI

Obama azuru kijiji alichozaliwa baba yake, awapongeza viongozi wa kisiasa

Rais wa zamani wa Marekani Barrack Obama amepongeza hatua ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuamua kuweka pembeni uhasimu wao na kushirikiana kwa ajili ya umoja wa taifa hilo.

Rais wa zamani wa Marekani Barrack Obama akiwa na bibi yake Sarah Obama na dada yake Auma Obama wakiwa Kogelo Magharibu mwa Kenya Julai 16 2018
Rais wa zamani wa Marekani Barrack Obama akiwa na bibi yake Sarah Obama na dada yake Auma Obama wakiwa Kogelo Magharibu mwa Kenya Julai 16 2018 twitter.com/KTNNews
Matangazo ya kibiashara

Obama ametoa kauli hii, wakati wa ufunguzi wa kituo cha kukuza michezo na kutoa elimu kwa vijana kinachofahamika kama Sauti Kuu kinachomilikiwa na dada yake Dokta Auma Obama, katika kijiji cha Kogelo, alikozaliwa baba yake, Magharibi mwa nchi hiyo.

Kiongozi huyo wa zamani ambaye amerejea nchini Kenya, kama raia wa kawaida, amesema ushirikiano unaoneshwa na viongozi wa nchi hiyo, ni dalili nzuri ya nchi hiyo kupata maendeleo.

“Kenya imepiga hatua kubwa sana. Ina Katiba mpya, kuna jitihada za uwezekezaji, na licha ya changamoto za kisiasa, Kenya sasa ina rais na kiongozi wa upinzani ambao wameamua kujenga madaraja,” amesema Obama.

Pamoja na hilo, Obama ameongeza kuwa vita dhidi ya ufisadi vitasaidia pakubwa kuimarisha uchumi wa nchi hiyo na kuhakikisha kuwa wananchi wote wanakuwa kuwa nafasi sawa bila kujali makabila wanayotokea.

Akiwa Kogelo, Obama ametembelea kaburi alikozikwa baba yake Hussein Obama lakini pia kukutana na ndugu zake wa karibu akiwemo bibi yake Sarah Obama.

“Nilipotembelea kaburi la baba yangu, lilinipa faraja kubwa ambayo siwezi kuipata katika hoteli yoyote ya kifahari,” aliongeza Obama.

Obama aliyewasili nchini Kenya mwishoni mwa wiki iliyopita na kukutana na rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, anazuru pia Afika Kusini kuhudhuria kongamano muhimu kuhusu rais wa zamani Nelson Mandela.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.