Katika ziara hiyo Obama aliyekuwa rais wa marekani kutoka 2009 hadi 2017, atatembelea Mji wa Kisumu na pia kijiji cha Kogalo, ambapo ni asili ya baba yake Hussein Obama Senior.
Aidha katika ziara hiyo, rais Obama atakutana na kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga na pia atazindua miradi kadhaa ya kuwasaidia vijana ikiwemo kituo cha mafunzo ya ujasiriamali na michezo