sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Mazungumzo ya amani kuanza Sudan, rais …
Rais wa DRC Felix Tshisekedi akiwa na mwenyeji wake rais wa Tanzania John Magufuli. 13 Juni 2019
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/06 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/06 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/06 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Naibu Spika wa bunge la Tanzania atangaza kuwania ubunge 2020

media Naibu Spika wa bunge la Tanzania, Dr. Tulia Ackson Mwansasu Gazeti la Jamhuri

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dr. Tulia Ackson Mwansasu ametangaza kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu wa Tanzania uliopangwa kufanyika 2020.

Mwanasiasa huyo kwa sasa ni mbunge wa kuteuliwa na rais na anashikilia madaraka ya unaibu spika tangu mwaka 2015.

Skizungumza na gazeti la kila siku nchini Tanzania la Mtanzania, Dr. Tulia, aliyepata kuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema atagombe ubunge mwaka 2020 lakini ameshindwa kuweka wazi ni jimbo gani atakalowania.

"Wengi wamekuwa wakihoji kwamba je, nina nia ya kugombea? ngoja niondoe sintofahamu hii, ni kweli nitagombea lakini bado sijajua nitagombea wapi,"ameeleza katika mahojiano na waandishi Mkoani Mbeya, Kusini Magharibi mwa Tanzania.

Wafuatiliaji wa mambo ya siasa nchini Tanzania wanasema huenda msomi huyo akawania ubunge katika jimbo la Mbeya Mjini au Rungwe.

Jimbo la Mbeya Mjini linaongozwa na Joseph Mbilinyi 'Sugu' wa Chadema wakati jimbo la Rungwe linaongozwa na Sauli Amon kutoka Chama cha Mapinduzi, CCM

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana