Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/04 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Umoja wa Mataifa kupiga kura vikwazo vya silaha Sudan Kusini

media Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha vikwazo dhidi ya Serikali ya Sudan Kusini mwishoni mwa mwezi Mei hadi Julai 15 na kuweka viongozi sita wa juu wa Sudan Kusini kwenye "orodha ya watu wanaokabiliwa na vikwazo" vya Umoja wa Mataifa. REUTERS/Andrew Kelly

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kupiga kura Ijumaa wiki hii azimio la rasimu, lililowasilishwa na Marekani, linalolenga kuweka vikwazo vya silaha dhidi ya Sudan Kusini, kwa mujibu wa wanadiplomasia kutoka baraza hilo.

Marekani inaungwa mkono na baadhi ya nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Baraza hilo lina wajumbe kutoka nchi kumi na tano15. Kwa hiyo Marekani inaungwa mkono na wanachama wa kutosha katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wanadiplomasia hao wameongeza.

Azimio hilo linahitaji kura tisa ili liweze kupitishwa na hakuna kura ya turufu itakayotumiwa.

Wajumbe watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa- Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi na China - wana kura ya turufu, na nchi zote hizo haziwezi kupinga azimio hilo.

Mkataba wa amani ulisainiwa mwezi uliopita nchini Sudan Kusini na ni jaribio la pili la wapatanishi kutoka Afrika Mashariki ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilianza mnamo mwaka 2013 na vimesababisha maelfu ya watu kuuawa.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe ni hasa kati ya kundi la kabila la Dinka, la Rais Salva Kiir na kabila la Nuer, anakotoka Makamu wa zamani wa rais na kiongozi wa waasi, Riek Machar.

Wajumbe kadhaa wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanaamini kwamba huu sio wakati mzuri wa kupiga kura kwa azimio hilo, wanadiplomasia wamesema, na kuna uwezekano wajizuie kupiga kura ya leo Ijumaa.

Mnamo mwaka 2016, azimio la rasimu ya Marekani ya kuiweka vikwazo vya silaha Sudan Kusini halikupata kura za kutosha.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha vikwazo dhidi ya Serikali ya Sudan Kusini mwishoni mwa mwezi Mei hadi Julai 15 na kuweka viongozi sita wa juu wa Sudan Kusini kwenye "orodha ya watu wanaokabiliwa na vikwazo" vya Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini umeona visa vya mauaji yaliyotekelezwa na vikosi vya serikali na washirika wao.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana