Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Kampuni ya CRBC yakabiliwa na tuhuma za ubaguzi Kenya

media Kampuni ya China Road and Bridge Corporation (CRBC) inayosimamia mradi wa reli ya Kati kutoka mjini Mombasa hadi Nairobi kwa muda wa miaka 10 yajikuta matatani kufuatia tuhum aza ubaguzi. Reuters/Thomas Mukoya

Wafanyakazi wa Shirika la Reli nchini Kenya, wanaofanya kazi katika mradi wa reli ya Kati kutoka mjini Mombasa hadi Nairobi, wanalalamikia ubaguzi kutoka kwa wakuu wa kampuni ya China Road and Bridge Corporation (CRBC) inayosimamia mradi huo kwa muda wa miaka 10.

John Chumo, Katibu Mkuu wa chama cha Wafanyakazi hao RAWU, amekiambia kituo kimoja cha habari nchini humo kuwa amekuwa akipokea malalamishi ya wafanyakazi wazawa kunyanyaswa kwa sababu ya rangi yao.

Aidha, amesema madereva wa treni hiyo ya mwendo kasi ambao ni raia wa nchi hiyo wanalipwa Dola 300 kwa mwezi huku wale wa China ambao wanafanya kazi sawa na wamefuzu kwa kiwango sawa, wakilipwa Dola 1,000.

“Ubaguzi huu wa malipo haikubaliki, kwa sababu kazi inayofanywa ni moja,” amesema Chumo.

Kutokana na tuhma hizi, Shirika la Reli nchini Kenya, limesema linaanzisha uchunguzi binafsi na kutoa saa 72 kwa viongozi wa kampuni hiyo ya China kujibu madai hayo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana