Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-RIEK MACHAR-SALVAR KIIR

Viongozi wa Sudan Kusini wakutana Mjini Kampala, kuendelea na mazungumzo ya kusaka amani

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar, wamekutana katika Ikulu ya Entebbe nchini Uganda kuendelea kuzungumzia amani ya nchi yao.

Rais wa Sudan, Omar Bashir akiwa na rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na kiongozi wa waasi Dr. Riek machar
Rais wa Sudan, Omar Bashir akiwa na rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na kiongozi wa waasi Dr. Riek machar REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Sudan Omar al Bashir, amehuhduhuria tena mazungumzo hayo, yaliyoongozwa na rais Yoweri Museveni.

Kwa saa kadhaa, viongozi hao wamekutana kwa siri wakijadiliana masuala mbalimbali, na mkutano huu umekuja baada ya viongozi wa Sudan Kusini kukubaliana kuhusu suala la usalama.

Siku ya Ijumaa, serikali na waasi walikubaliana kuondoa wapiganaji wake katika miji mbalimbali nchini humo ili kupata suluhu ya kudumu na kumaliza mzozo ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka minne sasa.

Mwezi uliopita, rais Kiir na Machar walitia saini mkataba wa kustisha vita kabisa nchini humo lakini saa chache baada ya kuanza kutekelezwa, ulivunjika baada ya pande hizo mbili kuanza kulaumiana baada ya mashambulizi mapya kushuhudiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.