Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Umoja wa Afrika waunga mkono Rwanda kuwania kwenye uenyekiti wa Francophonie

media Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo anatarajiwa kupambana na Mkuu wa sasa wa OIF, Michaelle Jean raia wa Canada, anayewania muhula wa pili. AFP PHOTO/ TONY KARUMBA

Viongozi wa Afrika waliokuwa wanakutana nchini Mauritania, wamekubaliana kuiunga mkono Rwanda kuongoza muungano wa nchi za dunia zinazozungumza lugha ya Kifaransa "La Francophonie" (OIF).

Waziri wa Mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo, anatarajiwa kupambana na Mkuu wa sasa wa muungano huo Michaelle Jean raia wa Canada, anayewania muhula wa pili.

Hivi karibuni rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliunga mkono Rwanda kuwania kwenye nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya ya nci zinazozungumza Kifaransa "Francophonie” (OIF). Baada ya rais Paul Kagame wa Rwanda kuzuru Ufaransa Jumatano wiki hii.

Uungwaji huu mkono kwa mgombea wa Rwanda kwenye nafasi hii ni ishara kubwa ambayo Ufaransa imeonyesha kwa nchi ya Rwanda. Emmanuel Macron alisema katika, kwa vitendo anataka kuonyesha nia yake ya kufufua uhusiano kamili na Rwanda.

Rwanda ni mwanachama wa Francophonie. Baadhi walifikia hata kuamini kwamba tulijitoa katika jumuiya hiyo, lakini sivyo. Tulijiunga na jumuiya nyingine, lakini sisi bado ni mwanachama wa Francophoni, alisema rais Paul Kagame wakati wa ziara yake nchi Ufaransa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana