Pata taarifa kuu

Umoja wa Afrika Kuwachukulia hatua viongozi wa juu wa Sudan Kusini

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika Mouusa Faki, anataka hatua kuchuliwa dhidi ya viongozi wa juu wa Sudan Kusini wanaosababisha kuvunjika kwa mkataba wa amani.

Wakimbizi wa ndani wa Sudani Kusini katika kambi ya Bentiu wakipokea chakula kutoka Umoja wa Mataifa, Juni 18, 2017.
Wakimbizi wa ndani wa Sudani Kusini katika kambi ya Bentiu wakipokea chakula kutoka Umoja wa Mataifa, Juni 18, 2017. REUTERS/David Lewis
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Faki, imekuja baada ya waasi nchini Sudan Kusini kuishtumu serikali kuvunja mkataba wa kusitisha mapigano ambao ulianza kutekelezwa siku ya Jumamosi.

Mkuu huyo wa AU, amesisitiza kuwa, huu ni wakati wa kuchukua hatua kwa sababu, viongozi wa Sudan Kusini wamekuwa na tabia ya kutoheshimu mikataba ya amani wanayokubaliana kutekeleza.

Wiki hii rais Salva Kiir na hasimu wake, Riek Machar walikubaliana kusitisha mapigano kabisa ndani ya saa 72, baada ya kukutana jijini Khartoum nchini Sudan, lakini utekelezwaji wa makubaliano hayo, upo mashakani.

Mapigano nchini Sudan Kusini yamekuwa yakiendelea kwa tangu mwaka 2015, na kusababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine kuyakimbia makwao.

Raia wa Sudan Kusini waliobaki nyumbani, wanakosa huduma muhimu kama chakula, maji safi na dawa na utekelezwaji wa mkataba wa amani ndio tumaini lao kuwa kutakuwa na utulivu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.