Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-SIASA-USALAMA

Makundi hasimu yatia saini mkataba wa amani Sudan Kusini

Makundi hasimu nchini Sudan Kusini yametia saini leo Jumatano mjini Khartoum, nchini Sudan, mktaba wa amani, huku wakikubaliana kusitisha mapigano ndani ya saa 72 zihazo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Al-Dirdiri Mohamed Ahmed amesema.

Kiongozi wa waasi Riek Machar (kushoto) na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kulia) wakati wa mazungumzo huko Khartoum na Rais wa Uganda Museveni na Rais wa Sudan al-Bashir (kati) tarehe 25 Juni.
Kiongozi wa waasi Riek Machar (kushoto) na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kulia) wakati wa mazungumzo huko Khartoum na Rais wa Uganda Museveni na Rais wa Sudan al-Bashir (kati) tarehe 25 Juni. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huu pia unaeleza kuachiliwa huru kwa wafungwa, utoaji wa misaada ya kibinadamu na kuundwa kwa serikali ya mpito ndani ya miezi minne.

Hata hivyo msemaji wa waasi amekataa baadhi ya vipengele vya mkataba huo.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar na viongozi wengine wa upinzani wamesaini mkataba huo wakati wa sherehe rasmi iliyofanyika hadharani mjini Khartoum.

Msemaji wa Riek Machar, hata hivyo, amesema waasi wamekataa kutumwa kwa waangalizi wa Umoja wa Afrika watakaofuatilia uheshimishwaji wa kusitishwa kwa mapigano, pamoja na mipango ya kutenga miji mitatu ambako idadra mbalimbali za serikali zitahamishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.