Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Salva Kiir na Riek Machar kukutana tena Jumatatu hii

media Rais Salva Kiir na mwenzake wa Sudani Omar Al Bashir. REUTERS/James Akena

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar wanatarajia kukutana tena Khartoum, nchini Sudani Jumatatu wiki hii kwa mkutano wao wa pili wa mazungumzo.

Viongozi hawa wanaendelea kukutana kwa lengo la kupata suluhisho la vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini mwao.

Mazungumzo hayo, ambayo yanafuata mkutano wa kikanda wa mataifa ya Afrika Mashariki (IGAD) nchini Ethiopia ili kufufua mchakato wa amani nchini Sudani Kusini, yatafanyika wakati ambapo Umoja wa Mataifa umetoa muda hadi mwishoni mwa mwezi Juni kwa makundi hasimu kuwa yamefikia " mkataba wa kisiasa unaofaa ", huku ukitishia kuwachukulia vikwazo.

Rais wa Sudani Omar al-Bashir anatarajia kuwa msimamizi wa mazungumzo hayo ya moja kwa moja kati ya viongozi hawa wawili wa Sudani Kusini mjini Khartoum, " kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudani.

Sudani itafanya kila kilio chini ya uwezo wake ili makundi hasimu nchini Sudani Kusini yafikie makubaliano ya kudumu, Wizara hiyo imeongeza.

Timu ya kiufundi kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki (IGAD), inayoendelea na jitihada za kuimarisha mchakato wa amani nchini Sudani Kusini, ilikua inatazamiwa kuwasili Khartoum mwishoni mwa juma lililopita, chanzo hicho kimesema.

Sudani Kusini ilipata uhuru kutoka Sudani mwaka 2011. Nchi hiyo ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwishoni mwa mwaka 2013 wakati Kiir alimshtumu makamu wake wa zamani, Riek Machar, kujaribu kumpindua madarakani.

Mgogoro uliosababishwa na wawili hao umesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na mamilioni ya watu kuyatoroka makaazi yao. Mamia ya maelfu wamekimbilia nchini Sudani kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana