Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-NKURUNZIZA

Wanne washikiliwa Burundi kwa madai ya uhujumu uchumi

Watu wanne raia Wa Ufaransa miongoni mwao Mrundi mmoja wametiwa nguvuni mwishoni mwa juma nchini Burundi kwa madai ya Utapeli kwenye sekta mawasiliano kama ilivyooeleza taarifa iliochapishwa Jumamosi na  wizara ya usalama nchini Burundi kupitia mtandao Wa kijamii Wa Twitter.

Raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza
Raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya wizara ya usalama imeeleza kuwa watu 4 raia Wa Ufaransa na mmoja raia Wa Burundi walikamatwa jijini Bujumbura kwa kosa la kuhujumu uchumi Wa Burundi kwa kuunda kampuni hewa ya mwasiliano na wanazuiliwa wakati huu uchunguzi ukiendelea.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Ikiriho uliokaribu sana na Utawala ambao umekuwa na taarifa nyeti, Wawili kati yao walikamatwa kwenye uwanja Wa ndege Wa mjini Bujumbura wakati wakiwa tayari kutoroka.

Duru za polisi nazo zinasema kuwa watu hao 5 wanatuhumiwa kosa la kughushi na utapeli katika sekta ya mawasiliano, na  walihojiwa na idara ya upelelezi ambayo ipo chini ya himaya ya rais kabla ya kupelekwa katika ,magereza mbalimbali nchini Burundi.

Jumamosi jioni kulikuwa na taarifa za kuachiwa huru kwa raia huyo Wa Burundi ambae ni miongoni mwa makada katika serikali Donatien Ndayishimiye ambae anazuiliwa katika jela kuu la Muramvya katikati mwa Burundi na baadae kurejeshwa jela, taarifa ambayo haikuthibitishwa.

Balozi Wa Ufaransa jijini Bujumbura hakupenda kuongea lolote kuhusu Sakata hili mbali na kuelewa kuwa anafuatilia kwa karibu.

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.