Pata taarifa kuu
KENYA-UNHCR-WAKIMBIZI-USALAMA-HAKI

UNHCR yaomba baadhi ya wakimbizi kupewa haki kamili Kenya

Wakati ulimwengu ukiadhimidsha Jumatano hii, Juni 20, Siku ya Wakimbizi ya Dunia, nchini Kenya wakimbizi bado wanaendelea kukabiliwa na matatizo mbalimbali. Kenya imewapa hifadhi takribani wakimbizi 500,000, hasa kutoka Somalia na Sudan Kusini.

Dadaab, kambi ya kwanza iliyofunguliwa mwaka wa 1991, tangu wakati huo imekuwa mji wa kambi ya wakimbizi.
Dadaab, kambi ya kwanza iliyofunguliwa mwaka wa 1991, tangu wakati huo imekuwa mji wa kambi ya wakimbizi. Sébastien Nemeth/RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika miaka ya hivi karibuni, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) limekua likiomba baadhi ya wakimbizi, hasa wale ambao wamekuwa wakiishi Kenya kwa zaidi ya miaka 30 kupewa haki kamili ya kuishi nchini humo.

Nchini Kenya, mfumo wa usimamizi wa wakimbizi ni ule wa wakimbizi kuwekwa katika kambi. Baadhi ya kambi kama vile Dadaab au Kakuma, kuna mamia ya maelfu ya wakimbizi. Wengi hawana haki ya kujielekeza sehemu yoyote ile au kufanya kazi. UNHCR imeomba wakimbizi hao waweze kupewa haki kamili.

"Wakimbizi ambao bado wana nguvu za kufanya kazi wanachangia uchumi," amesema Ivana Unluova, Naibu Mkurugenzi wa UNHCR nchini Kenya. Wachache sana hupata kibali cha kazi. Lakini ikiwa nchi itawapokea wakimbizi wengi, watalazimika kuanza kulipa kodi. Tunatarajia kwamba Kenya itachukua sheria mpya za kuimarisha utaratibu huu. "

Kwa upande wake Kodeck Makori, mkuu wa sekretarieti ya Wakimbizi nchini Kenya,anasema kuna watu ambao wanadai kuwa ni wakimbizi wakati si kweli.

"Wakimbizi pia wana haki ya kurudi nyumbani. Na lazima tuwawezesha kurudi. Wale wanaokuja sio wakimbizi wote wa kweli. Baadhi wanataka kutumia mfumo. Wanasema ni wakimbizi wakati si kweli, "Kodeck MAkori amesema.

Mnamo mwezi Septemba, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa unatarajiwa kupitisha makubaliano ya kimataifa kwa wakimbizi, kwa kuwapa haki kamili na ushirikiano wa kutosha. UNHCR inasubiri kuona ikiwa serikali ya Kenya itatekeleza hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.