Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-SALVA KIIR-AMANI

Rais wa Sudan aonya wanajeshi dhidi ya uasi

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, amewaonya maafisa wa jeshi kuacha tabia ya kuasi wanapoondoka jeshini.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Rais Kiir amelaani tabia ya Majenerali wanaondoka jeshini na kuunda makundi ya waasi au kuunda makundi mengine, wakiwa na matumaini ya kurejeshwa tena jeshini au serikalini.

Amewaambia wanaoasi wasalie msituni, wala wasifikirie tena kurejea jeshini.

Mwezi Aprilo, rais Kiir alitoa onyo hili na kuonya kuwa wale wanaoendelea kuunda makundi ya waasi watashughulikiwa ipasavyo.

Majenerali kadhaa waliokuwa katika jeshi la taifa hilo akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi Paul Malong, wameunda kundi la waasi.

Onyo la rais Kiir limekuja wakati huu, akitarajiwa kukutana na kiongozi wa waasi Riek Machar wiki ijyao jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.