Pata taarifa kuu
BEMBA-DRC-UBELGIJI-ICC

Jean Pierre Bemba awasili Ubelgiji

Aliyekuwa makamu wa raisi wa DRC Jean Pierre Bemba amewasili nchini Ubelgiji baada ya kuachiwa huru katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.

Aliyekuwa makamo wa raisi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean-Pierre Bemba.
Aliyekuwa makamo wa raisi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean-Pierre Bemba. REUTERS/JERRY LAMPEN
Matangazo ya kibiashara

Bemba aliyewahi kuwa kiongozi wa waasi,ambaye amekuwa mikononi mwa sheria kwa takribani muongo mmoja aliachiliwa kwa masharti maalum kwa mujibu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.

Katika uamuzi ulioshtua wengi juma lililopita majaji walimfutia mashtaka yaliyomkabili na kubadili adhabu yake ya kifungo miaka 18 jela kwa maelezo kuwa Bemba hawezi kuhukumiwa kwa makosa yaliyotekelezwa na majeshi yake nchini Afrika ya kati mwaka 2002-2003.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na mahakama Bemba aliondoka katika kizuizini ICC jumatano lakini bado yupo chini ya uangalizi wa mahakama na amewasili Ubelgiji kuungana na familia yake.

Nae wakili wa Bemba amethibitisha kuwasili kwa Bemba nchini humo.

Familia ya Bemba inaaminika kuishi katika kitongoji cha Rhode Saint Genese,kwenye umbali wa takribani kilomita 15 kusini mwa jiji kuu la Brussels ambako alikamatwa mnamo May 2008 kwa amri ya mahakama ya ICC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.