Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-MACHAR-KIIR

Rais Kiir na Machar kukutana tarehe 20 Juni jijini Addis Ababa

Mkutano wa kihistoria kati ya rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Dokta Riek Machar, umepangwa kufanyika tarehe 20 mwezi Juni jijini Addis Ababa, Ethiopia. 

Rais Salva  Kiir na Riek Machar, wakiwa Ikulu jijini Juba  mwaka 2016
Rais Salva Kiir na Riek Machar, wakiwa Ikulu jijini Juba mwaka 2016 REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya nchi wanachama za IGAD inasema kuwa mazungumzo haya yanalenga kuwafanya viongozi hao wawili kufikia makubaliano kwa mustakabali wa amabi na utulivu kwenye nchi yao inayokabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

IGAD inasisitiza kuwa tayari viongozi wote wawili wamepelekewa barua za mualiko na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.

Tayari upande wa Riek Machar umeshajibu barua hiyo na kuonesha utayari wa kushiriki, sawa na Serikai ya Juba ambayo hivi karibuni rais Kiir alisema haoni tabu ya kukutana na mpinzani wake.

Mazungumzo haya yanaenda kufanyika huku kukiwa na shinikizo kubwa kwa viongozi hawa wawili kufikia makubaliano au wakabiliwe na vikwazo kutoka jumuiya ya kimataifa.

Vita nchini Sudan Kusini imesababisha vifo vya watu zaidi ya laki 1 na raia wengine zaidi ya milioni 2 wamekuwa wakimbizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.