Pata taarifa kuu
UGANDA-JESHI-USALAMA

Jeshi la Uganda lathibitisha kumshikilia aliyekuwa Mkuu wa Polisi Kale Kayihura

Jeshi la Uganda UPDF limethibitisha kuwa linamshikilia aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo Jenerali Kale Kayihura.

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda Kale Kayihura
Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda Kale Kayihura Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Hilo limethibitishwa na msemaji wa jeshi hilo, Brigedia Richard Karemire, ambaye amesema Kayihura ameruhusiwa kuonana na Mawakili wake pamoja na familia yake.

Hata hivyo, jeshi halijaweka wazi sababu za kumshikilia Mkuu huyo wa Polisi,lakini kuna ripoti kuwa kukamatwa kwake huenda kunahusianana kuuawa kwa aliyekuwa msemaji wa jeshi la Polisi Andrew Felix Kaweesi.

Hali ya usalama nchini Uganda imeendelea kuwa mbaya katika siku za hivi karibuni, kutokana na mauaji na utekaji nyara wa raia wa nchi hiyo.

Wiki iliyopita, rais Yoweri Museveni alitangaza vita dhidi ya watu wanaotekeleza mauaji na utekaji nyara baada ya kumpiga risasi na kumuua mbunge wa chama tawala NRM Ibrahim Abiriga nje kidogo ya jiji la Kampala.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.