Pata taarifa kuu
BURUNDI-CAR-UN-USALAMA

Askari wa Burundi auawa Bambari, Jamhuri ya Afrika ya Kati

Askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) kutoka Burundi ameuawa katika eneo la Bambari, katikati mwa nchi hiyo. Askari huyo aliuawa wakati wa mapigano kati ya watu wenye silaha na askari wa Umoja wa Mataifa na jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa mujibu wa vyanzo vya Umoja wa Mataifa.

Askari wa vikosi vya Minusca nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakiwa katika moja ya operesheni dhidi ya makundi ya wapiganaji
Askari wa vikosi vya Minusca nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakiwa katika moja ya operesheni dhidi ya makundi ya wapiganaji UN Photo/Nektarios Markogiannis
Matangazo ya kibiashara

Askari wa Minusca kutoka Burundi aliuawa wakati wa mapigano na askari wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (Faca) amejeruhiwa, chanzo cha Umoja wa Mataifa huko Bambari ambacho hakikutaja jina kimeliambia shirika la habari la AFP.

Mapigano hayo yalitokea usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wiki hii.

Taarifa hii imethibitishiwa na shirika la habari la AFP na chanzo kingine cha Umoja wa Mataifa huko Bangui.

Msafara wa vikosi vya jeshi vya Jamhuri ya Afrika ya Kati (Faca), ambao ulikua njiani kuelekea Bangassou (kusini-mashariki) ambako wanajeshi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wangelitumwa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ulishambuliwa kwa risasi na kundi la watu wenye silaha katika eneo la Bambari.

Kwa mujibu wa AFP ikinukuu chanzo kutoka polisi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, msafara huo ulishambuliwa na kundi la wapiganaji la UPC. Chanzo hicho kimeongeza kwamba wapiganaji kadhaa wa kundi hilo waliuawa wakati wa mapigano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.