Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA

Kauli ya Nkurunziza yawashangaza wengi

Hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kwamba hatowania muhula mwengine katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 imeendelea kuibua mijadala mikubwa ndani na nje ya Burundi.

Rais Pierre Nkurunziza, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru katika uwanja wa P. Loius Rwagasore Bujumbura, Julai 1, 2015.
Rais Pierre Nkurunziza, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru katika uwanja wa P. Loius Rwagasore Bujumbura, Julai 1, 2015. AFP PHOTO / MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo ya Nkurunziza inakuja baada ya kuonyesha nia mapema ya kuendelea madarakani hasa katika kile alichokuwa akieeleza katika hotuba zake za nyuma kwamba alichaguliwa na Mungu kuhudumu. Lakini siku ya Alhamisi kauli ilibadilika na alipoeleza hatowania muhula mwengine katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Upinzani unajumuika katika muungano CNARED unasema mzozo wa Burundi sio Nkurunziza bali ni katiba ya Arusha ambayo imebadilishwa na kwamba anachokifnya Nkurunziza ni kuizubaza umma, kama anavyoeleza hapa Pancras Cimbaye msemaji wa Cenared.

Lakini swali tete ambalo limeendelea kuibuka ni kwanini rais Nkurunziza amebadili msimamo wake, na je ataheshimu kauli yake?

Wataalamu wanaona kuwa huenda ni kukosa uungwaji mkono wa viongozi wa ukanda, pamoja na mzozo wa ndan ya chama chake cha CNDD-FDD zikiwa ni miongoni mwa sababu za kubadili msimamo wake.

Hata hivyo wachambuzi wa maswala ya siasa wanaona kuwa kauli ya Nkurunziza inadhihirisha wazi kwamba hali ni tete upande wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.