Pata taarifa kuu
BURUNDI-KATIBA-SIASA-USALAMA

Rais Nkurunziza atia sahihi kwenye Katiba mpya

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ametia sahihi kwenye Katiba mpya tata. Sherehe ya utiaji sahihi imefanyika Alhamisi wiki hii katika ikulu ya rais mjini Gitega, katikati mwa Burundi. Katiba hii mpya iliyopitishwa Mei 17 katika kura ya maoni, inampa fursa ya Pierre Nkurunziza kusalia madarakani hadi mwaka wa 2034.

Sherehe ya utiaji sahihi imefanyika Alhamisi wiki hii katika ikulu ya rais mjini Gitega, katikati mwa Burundi
Sherehe ya utiaji sahihi imefanyika Alhamisi wiki hii katika ikulu ya rais mjini Gitega, katikati mwa Burundi Twitter.com
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii itafuatiwa na zoezi la kuitambulisha Katiba hii mpya. Zoezi ambalo litaanzia wilayani Bugendana, mkoani Gitega, ambapo Rais Nkurunziza anaelekea kuitambulisha kwa wakaazi wa wilaya hiyo.

Bugendana ndiko kulikozinduliwa rasmi mchakato wa katiba, lakini pia kampeni ya chama madarakani CN DD-FDD ya kuipiga debe katiba hiyo.

Wakati huo huo Rais Pierre Nkurunziza ametangaza kwamba hatowania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020.

Kwa upande wa upinzani, kupitishwa kwa Katiba hii mpya kumefuta mkataba wa Amani wa Arusha uliosainiwa mwaka 2000, ambao uliweka utaratibu wa kugawana madaraka kati ya makabila nchini humo.

Katiba hiyo mpya imeongeza muhula wa urais kutoka miaka mitano hadi saba.

Sheria hiyo mpya inaruhusu Nkurunziza kuwania mihula mingine miwili ya miaka saba kuanzia 2020, hivyo kumwezesha kusalia mamlakani hadi 2034.

Upinzani unasema kuwa katiba hiyo mpya inampa Rais Nkurunziza ambaye alitawazwa na chama chake cha CNDD-FDD 'Kiongozi wa Milele’ mapema mwaka 2018, kuvunja sheria anavyotaka bila kikwazo.

Katiba hii mpya ambayo inaanza kutekelezwa Alhamis wiki hii itageuza mambo mengi kwenye taasisi za maongozi ya taifa , lakini pia kutoa fursa kwa Rais Pierre Nkurunziza kuweza kuwania uongozi wa nchi hadi mwaka wa 2034.

Katiba hii pia inaanza kutekelezwa wakati mazungumzo ya amani yakiwa yamekwama baada ya serikali kukata kuketi meza moja na wapinzani. Kufuatia hali hiyo ya mkwamo,

Wajumbe wa Muungano wa Ulaya wamelichagiza Shirika la Umoja wa Afrika kuchukua mikononi mazungumzo ya amani ya Burundi kwa madai kwamba Jumuiya ya kimataifa imeanza kupoteza imani kwa mchakato wa upatanishi unaosimamiwa na Jumuiya ya Afrika ya mashariki na inayoongozwa na Rais Museveni pamoja na msuluhishi Benjamin Mkapa.

Nkurunziza, 54, amekuwa mamlakani tangu 2005. Utawala wake umekumbwa na misukosuko tangu 2015 baada ya kupuuzilia mbali mkataba wa kutowania urais tena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.