Pata taarifa kuu
KENYA-MAFUTA-UCHUMI

Kenya yaanza kusafirisha mafuta kutoka Lokichar kwenda Mombasa

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezindua rasmi usafirashaji wa mafuta kutoka eneo la Lokichar, Kaunti ya Turkana kuelekea bandari ya Mombasa.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akizindua usafirishaji wa mafuta katika eneo la Lokichar Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo Jumapili June 3 2018
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akizindua usafirishaji wa mafuta katika eneo la Lokichar Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo Jumapili June 3 2018 twitter.com/UKenyatta
Matangazo ya kibiashara

Kenyatta amesema mradi huu utasaidia kuinua uchumi wa taifa hilo, kutokana na ugunduzi wa mafuta katika eneo hilo la Kaskazini Magharibi.

Katika kipindi hiki cha mwanzoni pipa za mafuta 2,000 yatasafirishwa kwa barabara kila siku.

Hata hivyo, wakosoaji wanasema, mbinu hii ya kusafirisha mafuta umbali wa Kilomita 1,000 ni hatari na itachangia pakubwa kuharibika kwa barabara.

Hata hivyo, serikali ya Kenya imesema ujenzi wa bomba la mafuta utaanza hivi karibuni utakaomilikika kufikia mwaka 2021 ili kusafirisha mapipa 100,000 kila siku.

Mradi huu ulitarajiwa kuanza mwaka uliopita, lakini ukacheleweshwa kwa sababu ya tofauti ya namna ya  kugawana kwa mapato kati ya serikali kuu na ile ya Kaunti pamoja na wenyeji wa Lokichar.

Imekubaliwa kuwa serikali kuu itapata asilimia 75 ya mapato yote, huku asilimia 20 ikiiendelea serikali ya Kaunti ya Turkana, na asilimia tano, ikiwaendelea wakaazi wa Turkana.

Kenya imekuwa nchi ya kwanza, kuanza kuchimba na kusafirisha mafuta katika nchi za Afrika Mashariki.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.