Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-SALVA KIIR-RIEK MACHAR

IGAD: Hatima ya amani ya Sudan Kusini iko mikononi mwa rais Kiir na Machar

Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka Mataifa ya IGAD ambayo yamekuwa katika mstari wa mbele kusaidia kuleta amani nchini Sudan Kusini, sasa wanasema hatima ya nchi hiyo ipo mikononi mwa rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar.

Riek Machar(Kulia )  na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (Kushoto)  wakitia saini makubaliano mwaka 2014  jijini Addis Ababa
Riek Machar(Kulia ) na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (Kushoto) wakitia saini makubaliano mwaka 2014 jijini Addis Ababa REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Hili limebainika baada ya mkutano wa Mawaziri hao jijini Addis Ababa nchini Ethiopia wiki hii.

Mawaziri hao wamesema sasa viongozi wa mataifa ya IGAD wanajukumu la kumshawishi rais Kiir na Machar kukutana na kuzungumza ana kwa ana ili kuamua mustakabili wa nchi yao.

Mwakilishi kutoka nchini Kenya ambaye hakutaka kutajwa,Β  amesema imekuwa ni vigumu sanaΒ  kuwapatanisha wawakilishi wa pande hizo mbili na sasa hatima ipo kwa rais Kiir na Machar.

Hata hivyo, inavyoonekana haitakuwa rahisi kwa sababu tayari rais Kiir ameshasema hawezi kufanya kazi na Machar ambaye anaishi nchini Afrika Kusini.

Machar naye amekuwa akisema, amani ya kweli haiwezi kuwepo nchini humo iwapo rais Kiir ataendelea kuwepo madarakani.

Mazungumzo ya amani mwezi uliopita, yalimalizika kwa pande zote kutopata mwafaka wowote jijini Addis Ababa na kurejea nyumbani mikono mitupu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.