Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 15/10 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 15/10 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 14/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Mpaka wa Jaber/Nassib kati ya Jordan na Syria wafunguliwa (AFP)
 • Ufaransa: Dhoruba kali yasababisha watu watatu kufariki dunia Aude
E.A.C

IGAD: Hatima ya amani ya Sudan Kusini iko mikononi mwa rais Kiir na Machar

media Riek Machar(Kulia ) na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (Kushoto) wakitia saini makubaliano mwaka 2014 jijini Addis Ababa REUTERS/Goran Tomasevic

Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka Mataifa ya IGAD ambayo yamekuwa katika mstari wa mbele kusaidia kuleta amani nchini Sudan Kusini, sasa wanasema hatima ya nchi hiyo ipo mikononi mwa rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar.

Hili limebainika baada ya mkutano wa Mawaziri hao jijini Addis Ababa nchini Ethiopia wiki hii.

Mawaziri hao wamesema sasa viongozi wa mataifa ya IGAD wanajukumu la kumshawishi rais Kiir na Machar kukutana na kuzungumza ana kwa ana ili kuamua mustakabili wa nchi yao.

Mwakilishi kutoka nchini Kenya ambaye hakutaka kutajwa,  amesema imekuwa ni vigumu sana  kuwapatanisha wawakilishi wa pande hizo mbili na sasa hatima ipo kwa rais Kiir na Machar.

Hata hivyo, inavyoonekana haitakuwa rahisi kwa sababu tayari rais Kiir ameshasema hawezi kufanya kazi na Machar ambaye anaishi nchini Afrika Kusini.

Machar naye amekuwa akisema, amani ya kweli haiwezi kuwepo nchini humo iwapo rais Kiir ataendelea kuwepo madarakani.

Mazungumzo ya amani mwezi uliopita, yalimalizika kwa pande zote kutopata mwafaka wowote jijini Addis Ababa na kurejea nyumbani mikono mitupu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana