Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA

Upinzani kuandamana Jumanne nchini Zimbabwe

Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha MDC kimetoa wito kwa wafuasi wake kufurika mitaani siku ya Jumanne wiki ijayo kuomba marekebisho muhimu kwa kufanyika uchaguzi mkuu katika mazingira mazuri.

Tendai Biti, msemaji wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC)
Tendai Biti, msemaji wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC) (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe umepangwa kufanyika Julai 30.

"Tunajianda kufurika mitaa ya Harare siku ya Jumanne, wiki ijayo. Tunataka uchaguzi ulio huru, wa wazi na wa kuaminika," Tendai Biti, msemaji wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC), amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Siku ya alhamisi Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alitangaza kwamba uchaguzi mkuu umepangwa kufanyika Julai 30, uchaguzi ambao ni wa kwanza tangu kuondolewa madarakani mtangulizi wake Robert Mugabe mwezi Novemba mwaka jana baada ya kutawala nchi yo miaka thelathini na saba.

Emmerson Mnangagwa atapeprusha bendera ya chama cha Zanu-PF, madarakani tangu 1980, katika uchaguzi huo.

Chama cvha MDC kinataka kuhakikishiwa juu ya uhuru wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), hususan jeshi kuingilia uchaguzi huo, ukaguzi huru kwenye orodha ya wapiga kura, pamoja na haki sawa kwa vyombo vya habari vya umma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.