Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Kenyatta: Fedha zilizoibiwa zinapaswa kurejeshwa

media Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta. Reuters/Noor Khamis

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema wale wote wanaodaiwa kuiba fedha za umma zinazokadiriwa kuwa Dola Milioni 80 kutoka Shirika la huduma kwa vijana NYS, wabebe mizigo yao wenyewe na wasimlaumu yeyote.

Aidha, amesema serikali yake itahakikisha kuwa fedha zilizoibiwa zinarejeshwa.

Tayari washukiwa 24 kati ya 54 wamefikishwa Mahakamani, na kukanusha madai dhidi yao.

Watuhumiwa 24 walioshtakiwa kuhusiana na kashfa hiyo ya ufujaji wa pesa katika Shirika la Vijana wa huduma kwa Taifa (NYS) watakaa rumande kwa wiki moja. Uamuzi huo ulichukuliwa na jaji, ambaye

aliamuru wazuiliwe hadi wiki ijayo ambapo uamuzi wa kuachiliwa kwa dahamana utatolewa.

Miongoni mwa walioshtakiwa siku ya Jumanne ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Jinsia Lilian Mbogo Omollo na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Richard Ndubai.

Lilian Mbogo Omollo pia alikua afisa mhasibu wakati malipo hayo ya ulaghai yalipotolewa

Walikamatwa na wengine wakajisalimisha kwa polisi Jumatatu wiki hii na kisha kufikishwa mahakamni Milimani, Nairobi siku ya Jumanne wiki hii.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana