Pata taarifa kuu
TANZANIA-JOHN MAGUFULI-BIASHARA

Marekani, Saudi Arabia kushiriki maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam

Nchi zaidi ya 30 ikiwemo Marekani na Saudi Arabia zinatarajiwa kushiriki maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam yanayopangwa kuanza Juni 28 hadi julai 13 mwaka huu.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania (Tan Trade) Edwin Rutageruka akihojiwa na mwandishi wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka Mei 30, 2018
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania (Tan Trade) Edwin Rutageruka akihojiwa na mwandishi wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka Mei 30, 2018 Tan Trade
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kuhusu matayarisho Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania, Edwin Rutageruka ameiambia idhaa ya Kiswahili ya RFI kwamba baadhi ya nchi zitashiriki maonyesho hayo kwa mara ya kwanza.

“Maandalizi tayari yako ukingoni na tayari nchi 28 zimethibitisha kushiriki kama Japani, Saudi Arabia, Ujerumani na Marekani lakini tunafurahi sana kuja kwa Saudi Arabia kwa mara ya kwanza,”amesema Rutageruka

Saudi Arabia itashiriki kwa mara ya kwanza katika maonyesho hayo ambayo yaliasisiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1976.

Rutageruka amesema Mamlaka ya maendeleo ya biashara kwa kushirikiana na taasisi nyingine ikiwemo kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) na Shirika la Viwanda vidogovidogo (SIDO) zimekuwa zikishirikiana ili kuimarisha uzalishaji wa bidhaa bora za wafanyabiashara wa Tanzania ambazo zitakuwa na soko nje ya nchi.

Maonyesho ya biashara ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba ni fursa kwa wazalishaji na wafanyabiashara wa ndani ya Tanzania kuonyesha bidhaa wanazozalishwa kwa wanunuzi wa ndani na nje ya pia.

Mataifa jirani yatakayoshiriki katika Maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam ambayo hufanyika kila mwaka yakiwakutanisha wafanyabiashara wa ndani na nje ya Tanzania ni pamoja na mataifa yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.