Pata taarifa kuu
TANZANIA-HAKI ZA BINADAMU-MAGUFULI

Kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania (LHRC) chatangaza uteuzi wa mkurugenzi mpya

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) kimetangaza uteuzi wa Ana Henga kuwa mkurugenzi wake mkuu. Anachukua nafasi ya Dr. Hellen Kijo Bisimba ambaye amekiongoza kituo hicho kwa zaidi ya miaka 20.

Mkurugenzi mpya wa Kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania, Ana Henga (kushoto) akiwa na mkurugenzi anayemaliza muda wake Dr. Hellen Kijo Bisimba
Mkurugenzi mpya wa Kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania, Ana Henga (kushoto) akiwa na mkurugenzi anayemaliza muda wake Dr. Hellen Kijo Bisimba NYU RADIO OFFICIAL BLOG
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya kuteuliwa kuchukua nafasi hicho, Henga alikuwa mkurugenzi wa ushauri na maboresho wa kituo hicho ambacho kimekuwa mstari wa mbele katika utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania.

Kiongozi huyo mpya ni mhitimu wa shahada ya kwanza ya sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pia ana shahada ya uzamiri ya sera za maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na tovuti ya kituo hicho, Henga ana uzeofu katika masuala ya sheria na amefanya kazi katika kituo hicho tangu mwaka 2006 na LHRC inasema inaamini uteuzi wa mwanamama huyo utawezesha kufikia malengo la kuwa na jamii yenye usawa.

Kituo hicho kimekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za binadamu nchini Tanzania na hivi karibuni kilikuwa miongoni mwa taasisi sita zilizofungua kesi mahakama kuu ya Tanzania kupinga kanuni mpya za uongozaji wa vyombo vya habari vya mitandaoni.

Mkurugenzi anayemaliza muda wake Dr. Hellen Kijo Bisimba amenukuliwa na gazeti la kila siku la Mwananchi ametaja mambo mawili anayoyakumbuka katika uongozi wake kuwa ni mgomo wa madaktari uliotikisa nchi mwaka 2012 na tukio la kushindwa kuwasaidia watoto watatu wa kimasai waliokimbia jamii zao wakihofia kukeketwa.

Ripoti ya mwandishi wetu, Fredrick Nwaka

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.