Pata taarifa kuu
UGANDA-AJALI-USALAMA

Uganda yaomboleza vifo vya watu 22

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa, kufuatia vifo vya watu 22 baada ya ajali ya barabarani katika Wilaya ya Kiryandongo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mji mkuu wa Kampala Uganda, ambako, kama maeneo mengine ya nchi hiyo bendera zitapandishwa nusu mlingoti wakiomboleza vifo vya watu 22 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani.
Mji mkuu wa Kampala Uganda, ambako, kama maeneo mengine ya nchi hiyo bendera zitapandishwa nusu mlingoti wakiomboleza vifo vya watu 22 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani. (CC)/Wikipedia/Omoo
Matangazo ya kibiashara

Bendera zote nchini humo zinapepea nusu mlingoti kwa heshima ya watu hao. Ajali hiyo ilihusisha basi la abiria na Lori la mizigo.

Aidha, serikali itatoa Shilingi za nchi hiyo Milioni 5 kwa kila Familia kuisadia katika shughuli za mazishi.

Takriban watu 22 wakiwemo watoto watatu waliuwa kwenye ajali ya basia lililogonga tingatinga ambayo ilikuwa ikiendeshwa bila ya taa usiku kwa mujibu wa msemaji wa polisi Emilian Kayima ambaye aliongea na AFP.

Awali shirika la msalaba mwekundu lilisema kuwa jumla ya vifo ni 48 wakiwemo watoto 16.

Uganda ina kati ya rekodi mbaya zaidi za usalama wa barabara. Zaidi ya watu 9,500 waliuawa kwennye ajali za barabarani nchini humo kati ya mwaka 2015 na 2017 kwa mujibu wa takwimu rasmi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.