Pata taarifa kuu
MAFUGULI-TANZANIA-CHAMA CHA MAPINDUZI

Chama tawala nchini Tanzania charidhia kung'atuka kwa katibu mkuu wake

Chama tawala nchini Tanzania, Chama cha Mapinduzi (CCM) leo tarehe 28 Mei 2018 kimeridhia barua ya kustaafu kwa katibu mkuu wake Abdurahman Kinana.

Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akiwa na Abdurahman Kinana
Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akiwa na Abdurahman Kinana screenshot/Ikulu
Matangazo ya kibiashara

Kikao kilichoridhia kujizulu kwa Kinana, aliyedumu katika nafasi hiyo tkwa miaka saba kiliketi hii leo ikulu jijini Dar es Salaam na kuongozwa na mwenyekiti wa CCM Taifa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Taarifa iliyotolewa na Humphrey Polepole, Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi kwa vyombo vya habari imesema mwenyekiti wa CCM na rais wa Jamhuri amemshukuru Kinana kwa utumishi wake na kumtakia mafanikio katika shughuli zake.

“Napenda kukushukuru ndugu Kinana kwa utumishi wako kwa Chama cha Mapinduzi, CCM itaendelea kutumia uzoefu wake katika majukumu ya chama kwa kadri itakavyohitajika,”imesema taarifa hiyo.

Mchambuzi wa masuala ya siasa na mhadhiri wa chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dr. Benson Bana ameiambia RFI Kiswahili kuwa kuondoka kwa Kinana kunatoa fursa kwa watu wengine kukitumikia chama cha Mapinduzi na kuongeza kuwa Kinana atakumbukwa kwa mchango wake wakati chama hicho kilipokabiliana na upinzani mkali katika uchaguzi wa mkuu wa mwaka 2015.

Katika uchaguzi huo, CCM ilipata upinzani mkali kutoka kwa kada wake wa zamani Edward Lowassa ambaye alijiunga na upinzani na kuwania urais baada ya kutopitishwa na CCM.

Katika uchaguzi huo, Magufuli alishinda kwa asilimia 58 dhidi ya Lowassa aliyepata asilimia 39 ya kura.

Katika hatua nyingine kikao cha leo kiwachagua Afadhali Tabu Afadhali, Kombo Hassan Juma, Lailah Burhan Ngozi, Charles Makongoro Nyerere,Khadija Shaban Taya na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda kuwa wajumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya Taifa (NEC).

Kwa mujibu wa taarifa za chama hicho, kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kitaendelea kesho, jijini Dar es Salaam.

Ripoti ya  mwandishi wetu Fredrick Nwaka
 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.