Sintofahamu yaendelea kujitokeza kwa wanasiasa Kenya
Kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, Jumatano wiki hii anatarajiwa kurejea nchini mwake akitokea nchini Uingereza lakini safari hii huenda asipokelewe kama ilivyozoeleka na badala yake atakutana na shinikizo kubwa la kisiasa kuhusu wito wake wa kufanyika kwa marekebisho ya katiba.
Imechapishwa:
dinga anarejea ikiwa ni siku 3 tu zimepita tangu rais Uhuru Kenyatta atupilie mbali wito wa kufanyika marekebisho ya katiba hali inayozusha maswali kuhusu makubaliano yao ya Machi 9 ikiwa yatafanikiwa.
Hata hivyo makubaliano na wito huu ni mambo yanayoonekana kumkera naibu wa rais wa Kenya, William Ruto ambaye amewakejeli wanasiasa wanaotaka kutumia mgongo wa katiba kujinufaisha.
Tangu kushikana mikono kwa rais Kenyatta na Odinga wanasiasa nchini Kenya wamegawanyika huku baadhi wakiona makubaliano haya ni njama za kumtupa kando naibu wa rais Ruto.