Pata taarifa kuu
EU-BURUNDI-KURA YA MAONI

Matokeo rasmi ya kura ya maoni kutangazwa Burundi

Matokeo rasmi ya kura ya maoni iliyofanyika mwishoni mwa juma lililopita nchini Burundi yanatarajiwa kutangazwa Jumatatu wiki hii na Tume ya Taifa ya Uchaguzo (CENI), wakati huu kura ya ndio ikionekana kupita kufungua njia kwa rais Pierre Nkurunziza kusalia madarakani kwa miaka mingine 16 ijayo.

Maafisa wa tume ya Uchaguzi Burundi (CENI) wakihesabu kura.
Maafisa wa tume ya Uchaguzi Burundi (CENI) wakihesabu kura. REUTERS/Paulo Nunes dos Santos
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo mahakama ya katiba italazimika kuidhinisha matokeo hayo ambayo hata hivyo upinzani unaoongozwa na Agathon Rwasa ukisisitiza kutotambua matokeo hayo.

Upinzani umesema kura hiyo haikuwa huru wala ya haki na kwamba serikali kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi walishirikiana katika kutengeneza matokeo ya majimbo mengi nchini humo.

Serikali ya Burundi kwa upande wake imesisitiza kuwa kura hiyo ilifanyika kwa uwazi, uhuru na haki na kwamba madai ya upinzani wala ukosolewaji kutoka nje hayana msingi wowote kwa sasa.

Kura ya maoni nchini Burundi kuhusu marekebisho ya katiba imefanyika bila ya uwepo wa waangalizi wa kimataifa, huku ikiweka rehani mazungumzo ya amani yaliyokuwa yakiendelea na kusimamiwa na jumuiya za kikanda.

Nchi ya Burundi imefanya kura hii licha ya shinikizo na wito kutoka jumuiya ya kimataifa.

Muungano wa upinzani Amizero y' Abarundi kuna hatari upoteze nafasi zake serikalini, baada ya matokeo ya kura kutangazwa, kwani baada ya kuidinishwa na mahakama ya Katiba, rais Nkurunziza atakua na mamlaka kamili.

Hayo yanajiri wakati ambapo hali ya wasiwasi imeendelea kutanda nchini humo, bada ya mapigano makali kutokea siku ya umamosi mchana kati ya jeshi la serikali na kundi kubwa la wapiganaji lilioingia kutoka mashariki mwa DRC. Mapigano hayo yaliyodumu saa sita yalitokea kkwenye mlima mrefu wa Zina mkoani Bubanza magharibi mwa Burundi. Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote kuhusu mapigano hayo au hasara iliyotokea. Mashahidi wanasema wapiganaji hao walikua walivalia sare mpya ya jeshi la Burundi walifaulu kuingia katika msitu wa Kibira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.