Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-UNICEF-USALAMA-HAKI

Askari watoto 200 waachiwa huru kutoka makundi ya waasi Sudan Kusini

Shirika la umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limesema kuwa makundi yenye silaha nchini Sudan Kusini yamewaachia watoto zaidi ya 200 ambao walikuwa wanatumikishwa kama wapiganaji.

Askari watoto wakati wa sherehe ya kurejeshwa katika maisha ya kiraia Februari 10, 2015 Pibor, katika jimbo la Jonglei, Sudani Kusini, zoezi lililosimamiwa na UNICEF.
Askari watoto wakati wa sherehe ya kurejeshwa katika maisha ya kiraia Februari 10, 2015 Pibor, katika jimbo la Jonglei, Sudani Kusini, zoezi lililosimamiwa na UNICEF. AFP PHOTO/Charles LOMODONG
Matangazo ya kibiashara

Inakadiriwa kuwa watoto zaidi ya elfu 19 bado wanapigana kwenye makundi mbalimbali nchini humo.

Kuachiwa kwa watoto 210 kunafanya idadi ya watoto walioachiwa ndani ya mwaka huu peke yake kutoka kwenye makundi hayo kufikia 806, amesema msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq.

Umoja wa mataifa umesema kuwa unatarajia watoto zaidi kuachiwa siku za usoni ambapo jumla ya watoto elfu moja wataachiwa na makundi ya wapiganaji.

Farhan Haq amesema kuwa wengi wa watoto walioachiwa wanatoka kundi la waasi wa SPLM-IO huku 8 wakitoka kwenye jeshi la taifa la ukombizi.

Hata hivyo Umoja wa Mataifa umelaani kunyanyaswa kwa wafanyakazi wa mashirika ya misaada nchini Sudan Kusini, UN ikisema vurugu na vitendo vya kikatili vimezuia kufika kwa misaada ya kibinadamu kwa zaidi ya watu milioni 7.

Umoja wa Mataifa unasema jumla ya wafanyakazi wanne wameuawa na wengine 10 walitekwa nyara katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, huku ukisema upinzani na Serikali hawajafanya vyakutosha kusitisha mapigano na kuingilia kazi za wafanyakazi wa misaada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.