Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/04 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Kenyatta atia saini muswada tata kuhusu makosa ya mtandao

media Rais Uhuru Kenyatta akitia saini muswada kuhusuwa makosa ya mtandao. RFI-KISWAHILI

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametia saini muswada tata wa makosa ya mtandao kuwa sheria licha ya pingamizi kubwa kutoka kwa wanahabari na watetezi wa haki za binadamu.

Sheria hii mpya inawalenga wanahabari na wale wanaotumia mitandao ya kijamii watakaopatikana na kosa la kuchapisha habari za uongo lakini pia kwa watumizi wa mitandao mbalibali ya kijamii wanaosambaza picha za uchi.

Atakayevunja sheria hii mpya, atakamatwa na kufikishwa Mahakamani na kulipa faini ya Shilingi za nchi hiyo Milioni tano au kufungwa jela miaka miwili.

Lakini wale walio na tabia ya kuandika matusi au maneno ya kumdhalilisha mwingine pia watajipata matatani kwa mujibu wa sheria.

Mbali na hilo, yeyote atakayechapisha habari za uongo na kusababisha hofu au machafuko nchini humo, atafungwa jela miaka 10.

Hatua ya rais Kenyatta imekuja baada ya Kamati ya Kimataifa ya kutetea wanahabari CPJ, kutoa wito kwa kiongozi wa nchi hiyo kutotia saini sheria hiyo kwa sababu inalenga kuminya uhuru wa wanahabari.

Hata hivyo, wabunge wamejitetea na kusema kuwa sheria hiyo itasaidia kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao na uhalifu unaoweza kutokea na kusababisha uvunjifu wa amani katika taifa hilo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana