Pata taarifa kuu
KENYA-MAJANGA-ASILI

Idadi ya watu waliopoteza maisha Kenya yaongezeka na kufikia 41

Idadi ya watu walipoteza maisha baada ya kuvunjika kwa kingo za bwawa la maji katika eneo la Solai katika Kaunti ya Nakuru nchini Kenya, imefikia zaidi ya 40.

Afisa wa jeshi anatathmini uharibifu uliosababishwa na kuvunjika kwa kingo za bwawa karibu na mji wa Solail, Kenya, Mei 10, 2018.
Afisa wa jeshi anatathmini uharibifu uliosababishwa na kuvunjika kwa kingo za bwawa karibu na mji wa Solail, Kenya, Mei 10, 2018. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Mkasa huo uliotokea siku ya Jumatano usiku, wakati wakazi wa Solai wakiwa wamelala, umewaacha wengine zaidi ya 40 wakiwa na majeraha huku wengine wakiwa bado hawajapatikana.

Hii ndio mara ya kwanza nchi hiyo, kupatwa na mkasa huu katika kipindi ambacho mvua nyingi zimeendelea kunyesha na kusababisha mafuriko nchini humo na kusababia watu wengine zaidi ya 170 kupoteza maisha.

Awali Gavana wa mkoa wa Nakuru alisema kiwango cha uharibifu kinaendelea kutathminiwa na shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limetangaza kwenye Twitter kwamba limewaokoa watu 39.

Ripoti zinasema kuwa, nusu ya watu walipoteza maisha katika mkasa huo wa Solai ni watoto.

Mbali na maafa hayo, mamia ya watu wamepoteza makwao na kusalia wakimbizi baada ya tukio hilo, kwa mujibu wa shirika la Msalaba mwekundu

Tangu mwezi Machi, mvua hizo zimeua watu 132 na kusababisha zaidi ya watu 220,000 kuyahama makazi yao katika kaunti 32, serikali ya Kenya imesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.