Pata taarifa kuu
EU-BURUNDI-KURA YA MAONI

Umoja wa Ulaya wapinga mchakato wa marekebesho ya katiba Burundi

Umoja wa Ulaya umeendelea na msimamo wake wa kupinga mchakato wa marekebisho ya katiba unaoendelea nchini Burundi. Kura ya maoni kuhusu marekebesho ya katiba inatarajiwa kufanyika ifikapo Mei 17 mwaka 2018.

Mkuu wa sera za Umoja wa Ulaya Federica Mogherini, Septemba 20, 2017 huko New York.
Mkuu wa sera za Umoja wa Ulaya Federica Mogherini, Septemba 20, 2017 huko New York. REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Kura hii ya maoni itamruhusu Rais Nkurunziza kubaki madarakani hadi mwaka 2034.

Katika tangazo la Mkuu wa sera za mambo ya Nje za Ulaya Federica Mogherini lililotolewa siku ya Jumanne, Mei 8 linaeleza kwamba Umoja wa Ulaya haukubaliani na mazingira ambamo mchakato huu unaendeshwa, Umoja wa Ulaya umesema kuwa haukubaliani wala hautokubaliana na jaribio lolote la kuifanyia mabadiliko katiba ya Burundi. Umoja wa Ulaya ndio ulisimamia mkataba wa amani na usalama baina ya Warudi, uliosainiwa Arusha nchini Tanzania. Mkataba ambao ulipelekea kumalizika vita vya weyewe kwa weyewe vilivyo dumu muongo mmoja. RFI imesoma nakala hiyo.

Federica Mogherini ameshtumu mchakato ambao "unafanyika katika hali ya kutisha na ukandamizaji unaoendelea", akielezea "kuendelea kwa mauaji ambayo yanatekelezwa na baadhi ya maafisa wa serikali, watu kukamatwa kiholela bila hatia yoyote".

Mazungumzo ya kuindoa nchi hiyo katika mgogoro unaoendelea bado yanasitasita kwa miaka mitatu sasa kufuatia uamuzi wa serikali wa kukataa kuketi kwenye meza ya mazungumzo na upinzani ulio uhamishoni. Federica Mogherini ameelezea masikitiko yake kuwa mchakato huo "umekabiliwa na visa vya unyanyasaji na vitisho kwa wapinzani wa serikali". Amepongeza "jitihada za usuluhishi" za Jumuiya ya Mataifa ya Afrika Mashariki na za Umoja wa Afrika.

Hatimaye, wachambuzi wanaamini kuwa marekebisho haya ya Katiba yanakuja kufuta mkataba wa amani uliyosainiwa mwaka 2000 Arusha. Federica Mogherini anakumbusha kwamba Umoja wa Ulaya ni moja ya waliosimamia mkataba huo. Ameitaka serikali ya Burundi "kuheshimu" mkataba huo uliyopelekea waasi wa zamani ambayo leo wako madarakani kufikia madaraka kwa amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.