Ndani ya miaka mitatu mfululizo zaidi ya vyombo saba vya habari vimefunga milango baada ya kudaiwa kutoa ripoti zinazoikosoa serikali ya Kigali au kudorora kwa uchumi.
Kati ya vyombo hivyo vya habari, vituo viwili vilitangaza kuikosoa serikali papo hapo vikanyanganywa leseni huku wanahabari wawili wakiripotiwa kuihama nchi hii.
Lakini je, wanahabari nchini wanasema uhuru wao uko hatarini.
“Nina wasiwasi kuwa, uhuru wa vyombo vya habari nchini humu ni mdogo, inawezekanaje kosa la mtu mmoja lisababishe chombo cha habari kunyanganywa leseni? Kusema kweli uhuru wa vyombo vya habari nchini Rwanda haupo< “ mmoja wa wahahabari ambaye hakutaja jina lake amesema.
Licha ya maoni hayo kutoka kwa wanahabari, tume huru ya vyombo vya habari nchini humu RMC inadai kwamba, uhuru wa vyombo vya habari nchini humu upo.
“Uhuru wa vyombo vya habari upo japokuwa siyo kwa asilimia mia moja. Na kuhusu ripoti zinazotolewa na kutuweka katika nafasi mbaya, mara nyingi zinatungwa kwa faida zao wenyewe, ” Cleophas Barore.
Hadi sasa ripoti za shirika la wanahabari wasiokuwa na mipaka zimeiweka Rwanda katika nafasi ya 156 kati ya nchi 180 zinazominya uhuru wa vyombo vya habari.