Octavien Ngenzi, 60, na Tito Barahira, 67, mnamo mwezi Juni, walioongoza kwa nyakati tofauti wilaya hiyo ya mashariki mwa Rwanda, wameendelea kukanusha ushiriki wao katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda.
Baada ya miezi miwili ya kesi hiyo, walikutwa na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la"uhalifu dhidi ya ubinadamu" na "mauaji ya kimbari", kwa "kuhusika kwao kwa kuandaa na kuratibu mauaji" yenye lengo la "kuteketeza kabila la Watutsi.
Hukumu hiyo ni ya pili na nzito kuchukuliwa na mahakama ya Ufaransa kuhusiana na mauaji hayo mwaka 1994 nchini Rwanda baada ya hukumu kifungo cha miaka 25 iliyotolewa na Mahakama ya Rufaa dhidi ya afisa wa zamani wa jeshi Pascal Simbikangwa kwa mauaji ya kimbari na kuhusika katika uhalifu dhidi ya ubinadamu.