Pata taarifa kuu
SUDAN-KUSINI-USALAMA

Mamia ya wanajeshi watoto waachiwa huru Sudan Kusini

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya watoto UNICEF, limethibitisha kuachiwa huru kwa watoto zaidi ya 200 waliokuwa wamesajiliwa kama wanajeshi katika makundi ya wapiganaji nchini Sudan Kusini.

Askari watoto wakati wa sherehe ya kupokonya silaha, uhamasishaji na kujiunga na familia zao Februari 10, 2015 huko Pibor, Jimbo la Jonglei, Sudani Kusini. Zoezi uliosimamiwa na UNICEF.
Askari watoto wakati wa sherehe ya kupokonya silaha, uhamasishaji na kujiunga na familia zao Februari 10, 2015 huko Pibor, Jimbo la Jonglei, Sudani Kusini. Zoezi uliosimamiwa na UNICEF. AFP PHOTO/Charles LOMODONG
Matangazo ya kibiashara

Watoto hao walikuwa kwenye Jeshi la National Liberation Movement (SSNLM) ambalo mwaka 2016 walitia saini makubaliano ya amani na serikali.

UNICEF nchini Sudani Kusini inahitaji dola za Marekani milioni 45 kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za kuwaachia watoto kwenye vikosi na kuwakutanisha watoto 19,000 na familia zao miaka mitatu ijayo.

Umoja wa Mataifa unasema kuna takriban watoto 19,000 ambao wanatumikia jeshi na wanamgambo nchini Sudani kusini.

Kwa mujibu wa chanzo kutoka UNICEF, watoto wakirejea nyumbani, wazazi wao watapatiwa msaada wa chakula kwa ajili ya kusaidia kupambana na upungufu wa chakula.

Kulingana na taarifa ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto, sasa jitihada zinafanyika kuhakikisha watoto wengine wanaachiwa siku za usoni, chanzo hicho kimeongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.