Pata taarifa kuu
SUDAN-KUSINI-MAZUNGUMZO-USALAMA

Kundi la waasi la Riek Machar ladai kudhibiti jimbo la Liech

Waasi wanaongozwa na aliyekuwa Makamu wa rais nchini Sudan Kusini Riek Machar wamesema wamefanikiwa kudhibiti jimbo lenye utajiri wa mafuta la Liech Kaskazini mwa Juba, kuelekea mzungumko mwingine wa mazungumzo ya amani. 

Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar, hapa ilikua mnamo Februari 2014, kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini.
Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar, hapa ilikua mnamo Februari 2014, kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa wakuu wa Juba na waasi hawajatoa idadi ya waliouawa kwenye mapigano yaliyosababisha kudhibitiwa kwa jimbo hilo.

Serikali ya sudan Kusini, kupitia kwa Waziri wa habari wa jimbo la Liech, Lam Tungwar, amekiri kuwa jimbo hili limeshambuliwa na waasi.

“Waasi walishambulia ngome yetu asubuhi ya leo yapata saa kumi usiku, “ Waziri Tungwar amesema.

Kwa upande wake msemaji rasmi wa jeshi la Sudan Kusini, Lul Ruai Koang, amedai kuwa shambulizi la ghafla la waasi lina madhumuni ya kuwafanya wajigambe kuwa wana nguvu za kijeshi kabla ya kuendelea tena kwa mazungumzo ya amani Tarehe 26 mwezi huu mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia.

“Waasi walifanya shambulizi lao la kijeshi dhidi ya majeshi ya serikali ili kuwapumbaza wanaohusika na kupatansisha pande zote mbili zinazozozana, “ msemaji wa jeshi la Sudan Kusini amesema.

“Wahusika” anaotaja msemaji wa jeshi la serikali ya Sudan Kusini, Lul Ruai Koang, ni wa wajumbe wa Jumuiya ya maendeleo kanda ya Afrika Mashariki (IGAD), lililoandaa mazungumzo ya amani Addis Ababa.

Kwa upande wa waasi, msemaji rasmi wa wapiganaji wa Riek Machar, Kanali Gabriel Lapol anathibitisha kuwepo kwa waasi kwenye jimbo hilo la Liech.

“Makamanda wetu wote wa kijeshi wameepiga kambi katika sehemu tuliodhibiti, ” amesema Kanali Lapol, huku akiongeza “tunamiliki kikamilifu sehemu hiyo”.

Kutokana na kuanguka mikononi mwa waasi kwa jimbo hilo, sasa wakuu wa Juba kupitia msemaji wa jeshi la serikali, Lul Ruai Koang, wanataka IGAD, kufanya uchunguzi wa kina kuhusu kilichotokea kwenye jimbo la Liech.

“Tunatoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka ili waliohusika, waliokiuka mapatano ya amani wachukuliwe hatua kali, “ amesema Bw Ruai Koang.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na maelfu wengine kulazimika kuyahama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.