Pata taarifa kuu
SUDAN-KUSINI-MAZUNGUMZO-USALAMA

Mazunguzo ya amani kuanza April 26 Sudan Kusini

Baraza la amani na Usalama la Umoja wa Afrika limekuwa jijini Juba nchini Sudan Kusini na kukutana na Baraza la Mawaziri kuelekea awamu nyingine ya mazungumzo ya amani tarehe 26 mwezi huu.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir katika Mkutano wa Igad Machi 25, 2017 Nairobi.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir katika Mkutano wa Igad Machi 25, 2017 Nairobi. SIMON MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Habari Michael Makuei amethibitisha kuwepo kwa mkutano kati ya serikali ya Juba na Baraza hilo lenye wajumbe 25.

Lengo la ziara hii ya siku tano ni kuweka shinikizo kwa serikali na makundi ya waasi, kusitisha mapigano na kuheshimu mkataba wa amani ili kumaliza vita vilivyoanza mwaka 2013.

Sudan Kusini imeendelea kukumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, mapigano ambayo yamesababisha vifo vya watu wengi na maelfu wengine kulazimika kuyahama makazi yao.

Sudan Kusini ilitumbukia katika vita hivyo mwaka mmoja baada ya kupata uhuru wake, kutokana na maslahi binafsi kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake Riek Machar, kwa mujibu wa mashirika ya kiraia nchini humo.

Maafisa kadhaa wa ngazi ya juu walilitoroka jeshi na kuamua kuanzisha vita vya maguguni dhidi ya rais Salva Kiir.

Mpaka sasa mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini hayajazaa matunda yoyote, kutokana na kila upande kujipendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.