Pata taarifa kuu
KENYA-KUJIUZULU-IEBC

Makamishena watatu wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya wajiuzulu

Makamishena watatu wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) wametangaza kujiuzulu nyadhifa zao.

Waliokuwa Makamishena wa Tume ya Uchaguzi  Paul Kurgat, Margaret Wanjala na Naibu Mwenyekiti   Consolata Nkatha wakati wakitangaza kujiuzulu kwao siku ya Jumatatu  Aprili 16 2018 jijini Nairobi.
Waliokuwa Makamishena wa Tume ya Uchaguzi Paul Kurgat, Margaret Wanjala na Naibu Mwenyekiti Consolata Nkatha wakati wakitangaza kujiuzulu kwao siku ya Jumatatu Aprili 16 2018 jijini Nairobi. COURTESY
Matangazo ya kibiashara

Wakiongozwa na Naibu Mwenyekiti wa Tume hiyo Connie Nkatha Maina, Margaret Mwachanya na Paul Kurgat wamesema wamefikia uamuzi huo kutokana na uhusiano mbaya kati yao na Mwenyekiti Wafula Chebukati.

Aidha, wamemshtumu Chebukati kwa kushindwa kutoa uongozi bora na kutatua changamoto zinazoshuhudiwa ndani ya Tume hiyo, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu tata wa mwaka 2017.

Wamepinga pia hatua ya Chebukati kumpa likizo ya lazima, Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Ezra Chiloba anayetuhumiwa kufanya makosa ya manunuzi wa vifaa mbalimbali vya Uchaguzi bila ya kuwashirikisha.

“Tume imekosa mwelekeo, kumekuwa na kutoaminiana,” amesema Margaret Mwachanya aliyesoma taarifa ya kujiuzulu kwao jijini Nairobi.

“Kuchukua hatua ya kumpa likizo Mkurugenzi wa Tume ni jambo ambalo linahitaji kila mmoja kuhusishwa,”.

“Mwenyekiti kwa muda mrefu amekuwa akishindwa kutoa uongozi bora na hivyo kukwamisha kazi ya Tume hiyo,” aliongeza.

Kujiuzulu kwa Makamishena hawa, kunaiacha Tume hiyo na Makamishena watatu Wafula Chebukati, Abdi Guliye, na Boya Molu.

Hii inaifanya Tume hiyo kutoendelea na majukumu yake kwa mujibu wa sheria kwa sababu Makamishena watano kati ya Sita ndio wanaohitajika ili kuendelea na majukumu mbalimbali.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa, itakuwa ni vigumu kwa Tume hiyo kuendelea na shughuli zake katika mazingira ya kisasa huku wakihoji kuwa, tofauti zilizoshuhudiwa ziliathiri matokeo ya Uchaguzi wa mwaka uliopita.

Kujiuzulu kwa Makamishena hao kumekuja wakati Mwenyekiti Chebukati alipokuwa anajiadaa kuongoza kikao cha dharura kujadili tofauti ndani ya Tume hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.