Pata taarifa kuu
RWANDA-KIMBARI-KAGAME

Rwanda:Baadhi ya mataifa ya Ulaya yamekataa kuwakamata waliochochea mauaji ya Kimbari

Rwanda imeyashutumu tena mataifa mbalimbali ya Ulaya kwa kushindwa kuwakamata watu waliohusika katika mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya Watutsi mwaka 1994.

Kumbukumbu ya maombolezo ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda mwaka 1994
Kumbukumbu ya maombolezo ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda mwaka 1994 www.newtimes.co.rw
Matangazo ya kibiashara

Shutuma hizo zimetolewa siku ya Ijumaa jijini Kigali wakati wa kutamatisha juma la kumbukumbu ya mauaj hayo mabaya katika historia ya nchi hiyo.

Katika hotuba yake, Mwenyekiti wa Baraza la Senate Benard Makuza amesema Rwanda haitovumilia nchi hizo.

Miongoni mwa nchi zinazoshutumiwa ni Ufaransa na licha ya juhudi za hapa na pale zinazofanywa kuimarisha uhusiano wa nchi hizi mbili.

Naye Waziri wa nchi katika Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Olivier Nduhungirehe amekiri kwamba, uhusiano baina ya ufaransa na Rwanda si mzuri.

“Uhusiano baina ya rwanda na ufaransa haujatengamaa kwani ufaransa bado inawapa hifadhi watu waliotekeleza mauaji ya kimbari na imeshindwa kuwapeleka mahakamani,” alisema.

Alipofungua juma la maombolezo wiki iliyopita, rais Paul Kagame alisema kwamba, licha ya kupita miaka mingi baada ya mauaji hayo, haimaanishi maovu yaliyofanywa dhidi ya watutsi, yamesahaulika.

Watu zaidi ya 800,000 walipoteza maisha baada ya mauaji hayo yaliyoishangaza dunia baada ya hatua ya haraka kutochukuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.