Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

Mazungumzo ya amani yaanza tena Sudan Kusini

Mazungumzo ya amani nchini Sudan Kusini yanaanza tena katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Abba. Mazungumzo hayo yanalenga kufikia amani ya kudumu na makubaliano ya kuachiliwa kwa aliye kuwa makamu wa rais Riek Machar, ambaye yuko katika kizuizi cha nyumbani nchini Afrika Kusini.

Juni 18, 2017,wakimbizi wa ndani wa Sudan Kusini wakipewa msaada wa chakula katika kambi ya Bentiu, kusini mwa Sudan Kusini..
Juni 18, 2017,wakimbizi wa ndani wa Sudan Kusini wakipewa msaada wa chakula katika kambi ya Bentiu, kusini mwa Sudan Kusini.. REUTERS/David Lewis
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yanaanza wakati ambapo makundi mapya ya waasi yanaendelea kuundwa.

Aliyekuwa Mkuu Majeshi nchini humo ameunda jipya kundi la waasi. Paul Malong ambaye alitimuliwa katika wadhifa wake na Rais Salva Kiir mwaka uliyopita, amechukua hatua hiyo dhidi ya utawala wa Kiir.

Malong ambaye amekuwa akiituhumu serikali kwa rushwa na makosa yamengine ya ufisadi, amesema kuwa kundi lake litakuwa na jukumu kubwa la kuiondoa Sudan Kusini kwenye sintofahamu na kuielekeza katika demokrasia na maendeleo.

Malong alituhumiwa mara kadhaa na Umoja wa mataifa kwa kuratibu mashambulizi ya kikabila dhidi ya raia.

Sudan Kusini imeendelea kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Vita hivyo vilianza mwaka mmoja tu baada ya taifa hilo changa kujipatia uhuru wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.