Pata taarifa kuu
RWANDA-MAADHIMISHO

Rwanda kuhakikisha mauaji ya Kimbari hayajirudii

Raisi wa Rwanda Paul Kagame amesema ukweli na kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 dhidi ya watutsi vitabaki kuwa msingi wa kujenga taifa na kuwasaidia wanyarwanda kuikabili historia yao na kujisahihisha katika kulirejesha taifa hilo katika uimara wake.

Mauaji ya kimbari yaligharimu maisha ya watu wasipopungua 800 000 kati ya mwezi Aprili na Julai 1994.
Mauaji ya kimbari yaligharimu maisha ya watu wasipopungua 800 000 kati ya mwezi Aprili na Julai 1994. Β© REUTERS/Finbarr O'Reilly
Matangazo ya kibiashara

Raisi Kagame aliyasema hayo katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaliyofanyikia Gisozi ambapo Kagame na mkewe Bi Jeannette Kagame walijumuika na wanyarwanda na marafiki wa Rwanda kuzindua wiki ya maadhimisho ya mauaji ya halaiki dhidi ya watusti.

Maadhimisho hayo yalianza kwa matembezi ya amani katika jiji la kigali.

Kagame amesema historia ya Rwanda inakumbusha kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha mauaji ya halaiki hayatokei tena nchini humo bali wanyarwanda wakihimizana kulijenga taifa na kuimarisha mshikamano baina yao.

Wanyarwanda na marafiki wa Rwanda wameanza shughuli za wiki kwa kumbuka mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi, miaka 24 baada ya mauaji yaliyogharimu maisha ya zaidi ya watu milioni katika siku 100.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.