Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/04 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/04 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka
Kundi la Islamic State (IS) ladai kuhusika na mashambulizi nchini Sri Lanka bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi (Amaq)
E.A.C

Serikali ya Rwanda kuwatia ndani ombaomba mjini Kigali

media Shughuli mbalimbali zikiendelea mjini Kigali nchini Rwanda RFI/Stéphanie Aglietti

Serikali ya Kigali imetangaza kuwawinda vikali na kuwaweka gerezani walemavu wote wanaojihusisha na vitendo vya kuomba omba barabarani Kwa madai kuwa ni chanzo cha uchafu mjini hapo na uamzi huo umepokelewa kwa shingo upande miongoni mwa walemavu.

Uamuzi huo ambao unaweza kutekelezwa wakati wowete kuanzia sasa umewaonya walemavu hao kuwa kama hawatositisha shughuli uombaji, watatiwa ndani.

Kwa upande wa walemavu wamepokea umamuzi huo kwa ushingo upande huku baadhi ya raia wakisema kwamba uamuzi huo umekuja kwa lengo la kukandamiza walemavu na watu maskini.

Huku hayo yakiarifiwa, mashirika ya kiraia nchini Rwanda yameshauri kwamba, kabla ya utekelezaji hatua hiyo kufanywa kungekuwepo kwanza mazungumzo ya pande zote.

Licha ya hatua hiyo kuzua minong’ono lukuki miongoni mwa wakazi wa jiji hilo, polisi ya Rwanda imedai kama mji wa Kigali utaomba msaada, wako tayari kutekeleza kazi yao ipaswavyo kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la polisi mjini Kigali Hitayesu Emmanuel.

Ripoti mbalimbali mbalimbali zimekuwa zikiitaja Kigali kuwa miongoni mwa miji safi barani afrika huku ripoti zingine hususani zile za kutetea haki za binadamu, zikiishutumu Kigali kwa kuwafunga watu wasiojiweza.

 

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana