Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Tume ya Ukweli na Maridhiano yatoa ripoti yake Burundi

media Askofu Jean-Louis Nahimana, Mwenyekiti wa Tume ya Ukweli na Maridhiano Burundi (CVR). RFI/ Esdras Ndikumana

Tume ya Ukweli na Maridhiano (CVR), inayopingwa na upinzani na vyama huru vya kiraia nchini Burundi, imetoa ripoti yake, zaidi ya miaka mitatu baada ya kuundwa kwake.

Tume hii inabakiza miaka miwili tu ya kufanya kazi yake ngumu kutoa mwanga kuhusu uhalifu mkubwa uliotekelezwa nchini humo tangu uhuru wake hadi mwaka 2008. Nusu karneiliogubikwa na mauaji mengi ya kikabila.

Tume ya Ukweli na Maridhiano nchini Burundi haijaweza kupata msaada kutoka jumuiya ya kimataifa, ambayo inabaini kwamba haitoweza kuendesha kazi hiyo kwa ubora zaidi wakati ambapo Burundi inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa tangu Pierre Nkurunziza alipochukua uamuzi wa kuwania muhula wa tatu mnamo mwaka 2015. Lakini Tume hii imebaini kwamba imeridhika na kazi nzuri iliyofanya.

Mwenyekiti wa tume hiyo Askofu Jean-Louis Nahimana amesema waliweza kuwasikiliza watu 60 000 waliotendewa maovu au ndugu wa waliotendewa maovu, waliweza kuorodhesha watu 70,000 waliotendewa maovu, watuhumiwa 13,000 walitambuliwa na makaburi ya halaiki 3,500 yaligunduliwa.

Askofu Jean-Louis Nahimana amehakikisha kuwa miaka mitatu baada ya kuteuliwa kwa tume yake, ripoti inaonyesha kazi nzuri tume iliyoifanya.

"Lakini mambo hayajakuwa rahisi. Kwa mfano, Zoezi la kuwasikiliza waathirika na ndugu wa waathirika lilichukua miezi miwili. Zoezi hili lililoanza baada ya kuchelewa miaka miwili lilidumu zaidi ya mwaka mmoja, " amesema Askofu Nahimana.

“Licha ya uwezo mdogo ambao tunao, kazi yetu ilikwenda vizuri kabisa. Kwa hiyo tumepata matokeo mazuri, " Askofu Nahimana ameongeza.

Mwenyekiti wa Tume ya Ukeli na Maridhiano nchini Burundi ana imani kwamba kazi ya tume hiyo inaweza kusaidia Burundi kukomesha vurugu za mara kwa mara zinazoendelea kuikumba nchi hiyo tangu uhuru wake mwaka 1962.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana