Pata taarifa kuu
BURUNDI-UNSC-SIASA-USALAMA

Baraza la usalama: Tuna wasiwasi na hali inayoendelea Burundi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Burundi kushirikiana na upinzani katika kuandaa uchaguzi unaopangwa kufanyika nchini humo mnamo mwaka wa 2020.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (Kushoto) na mkewe Denis Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (Kushoto) na mkewe Denis Nkurunziza wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii ilitolewa siku ya Jumatano,wakati ambapo baraza hilo likionyesha wasiwasi wake kuhusu hali ya kisiasa nchini humo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekua likiinyoa serikalia ya Burundi kuhusu hali ya kisiasa na kibinadamu inayoendelea kushuhudiwa nchini humo, wakati ambapo watu wanaendelea kupotezwa na wengine kuuawa na miili yao kutupwa mitoni au katika ziwa Tanganyika. Maafisa wa usalama na wale wa Idara ya ujasusi pamoja na vijana wa chama tawala CNDD-FDD, Imbonerakure, wamekua wakinyooshewa kidolea kuhusika na vitendo hivyo viovu.

Baraza hilo la Umoja wa Mataifa pia limeonya kuhusu upatikanaji wa mwafaka katika mazungumzo ya amani ya Burundi yanayoongozwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki huku likiitaka Serikali ya Burundi kulishughulikia suala hili, ripoti iliyoainishwa na wanachama 15 wa ngazi za juu ya Umoja wa Mataifa imesema.

Katika ripoti hiyo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linasema mazungumzo ya amani na Wapinzani ndio njia pekee kuhakikisha Uchaguzi unaopangwa Kufanyika mwaka 2020 unakuwa huru, wa haki, na wazi,

Hayo yanajiri wakati rais wa Burundi Pierre Nkurunziza akiwatahadharisha wanasiasa wa Upinzani ambao wamekuwa wakipiga kampeni kuwataka wananchi kupiga kura ya Hapana, wakati wa kura ya maoni ya mwezi ujao nchini humo.

Mgogoro wa kisiasa nchini Burundi umesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao na kukimbilia katika nchi jirani. Mgogoro huo pia umesababisa zaidi ya watu 2000 kupoteza maisha yao kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadamu nchi humo na yale ya kimataifa.

Kambi ya wakimbizi ya Nduta nchini Tanzania, inayowapa hifadhi wakimbizi kutoka Burundi
Kambi ya wakimbizi ya Nduta nchini Tanzania, inayowapa hifadhi wakimbizi kutoka Burundi MSF

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.