Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/04 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka
Kundi la Islamic State (IS) ladai kuhusika na mashambulizi nchini Sri Lanka bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi (Amaq)
E.A.C

Kenya yamfukuza kwa mara nyingine mwanaharakati Miguna Miguna

media Mwanasheria na mwanaharakati wa vuguvugu la upinzani nchini Kenya, Miguna Miguna akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta. 26.03.2018. REUTERS/Stephen Mdunga

Mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Kenya na mwanaharakati wa muungano wa upinzani wakili Miguna Miguna siku ya juma hili amefurushwa tena nchini humo ikiwa ni mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili, mwanasheria wake amesema.

Miguna Miguna mwanaharakati wa muungano wa upinzani wa NASA, alisafirishwa kwa nguvu kurejeshwa nchini Canada mwezi uliopita.

Mahakama kuu ya Kenya Februari 26 mwaka huu iliiagiza idara ya uhamiaji kumruhusu Miguna kurejea nchini humo na alireja Jumatatu ya wiki hii.

"Amefukuzwam," kwa mara ya pili, amesema wakili wake Cliff Ombeta alipozungumza kwa njia ya simu.

"Ilikuwa ni ndege iliyoelekea Dubai lakini hatujui ni wapi wanampeleka."

Mtoa taarifa kwenye uwanja wa ndege amethibitisha kufurushwa tena kwa miguna baada ya idara ya uhamiaji kumkatalia kuingia nchini Kenya licha ya jaji wa mahakama kuu kuagiza aachiliwe na kumuwasilisha mahakamani siku ya Ijumaa.

Kufukuzwa kwa mara ya kwanza kwa Miguna kulikuja baada ya kukamatwa kutokana na kushiriki sherehe za kuapishwa kwa kinara wa upinzani Raila Odinga ambaye anasisitiza yeye ni rais wa watu.

Wizara ya mambo ya ndani imesema kuwa Miguna "alikana" uraia wake baada ya kuchukua uraia wa Canada miaka michache iliyopita.

Uraia wa nchi mbili unaruhusiwa kisheria nchini Kenya, na mwezi Agosti Miguna aliwania ugavana wa jiji la Nairobi akiwa na ushahidi kuthibitisha yeye ni raia wa Kenya.

Miguna hajashika nafasi yoyote ya uma lakini amejitangaza kama jenrali wa vuguvugu la kushinikiza mabadiliko na kuipinga Serikali, akiwajibika na utekelezaji wa maazimio ya kuipinga Serikali yaliyotangazwa na upinzani.

Kufurushwa kwa Miguna ni muendelezo wa mzozo wa kisiasa nchini Kenya tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi na mahakama ya juu kwenye uchaguzi wa mwezi Agosti na baadae Odinga kususia uchaguzi wa marudio wa Octoba ambao ulimpa ushindi rais Uhuru Kenyatta.

Taarifa ya shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch iliyotolewa Jumatatu ya wiki hii, ilidai kuwa watu 104 wamekufa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi na makundi mengine ya wapiganaji.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana